MLEVI NA MCHUNGAJI WAMEKUTANA;
MCHUNGAJI; "Unakunywa bia!?
MLEVI; "Ndio.
MCHUNGAJI; "Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; "Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; "Bia moja bei gani!?
MLEVU; "2500/
MCHUNGAJI; "Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; "Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; "Ndio!
MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; "Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; "Uliza!
MLEVI; "Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; "Hapana!
MLEVI; "Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; "akasepa"
MLEVI AKIWA BAR:
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni "nikusaidie nini?"
MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia
Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo... teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu
WALEVI WAWILI:
Walevi wawili waliokota kioo, mlevi wa 1 akaangalia muda mrefu kisha akasema "hii sura sio ngeni machoni mwangu sema jina tu silikumbuki..! !!
Mlevi wa pili akamnyang'anya kisha nae akaangalia kioo akasema "wee kweli huna akili, si mimi huyu? halafu unajidai hunikumbuki ...!!!
MLEVI NA JAMAA:
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
0 comments:
Post a Comment