Maroli mengi ya mizigo yalisimama msamvu morogoro, miongoni mwa maroli hayo yaliyosimama! Walipaki dereva mzee Boaz na utingo wake Erik, baada ya kuegesha roli lao mzee Boaz alimtuma Erik .....
"Erik nenda kamwangalie shemeji yako"
"Nimwambie aje au utakwenda?"
"Toka lini mm nikaenda?, mwambie nimeshafika",
Erik alikwenda mpaka alikoagizwa na kukuta mlango umefungwa kwa kufuli. Lakini majirani au wapangaji wengine walikuwepo kwenye nyumba hiyo.....
"Salama jaman?"
"Salama,karibu"
"Asante vp huyu bibie katoka?"
"Teh! Teh! Halooooo"
walicheka majirani
" kha! Sasa mbona wanacheka?" Eriki alijiuliza....
"Basi akija mwambien mzee boaz anamtaarifu kwamba amewasili hapa msamvu"
" mzee Boaz ni nani?" Mpangaji mmoja aliuliza
"Dereva wangu"
" mzee daudi je?" Mpangaji mwengne akadakia
"Huyo simjui"
Wale wapangaji wakatazamana tena, wakacheka kama mwanzo....
"Basi akija tutamwambia, wala usitie shaka,
Wakati shabani anatoka kuelekea alipotoka nje akakutana na bajaji,, akiwa anashuka Paulina ambaye ndo haswa alikuwa amemfuata!,,
Alivaa kisket kilichomfika juu ya mapaja huku akikivuta ili angarau kimfike juu ya magoti...
"Vipi erik?"
"Mzee anakuita"
" kafikia wapi?"
"Kulekule kwa siku zote"
"Kaja na mzigo wangu lkn"
"Mi sijui"
"Basi njoo kwanza chumbani nibadili nguo alafu twende"
Erik alimfuata Paulina kwa nyuma huku akifumba macho kwan alijua ni Mali ya dereva wake, Yeye kama utingo hatakiwi kumgusa popote,
Paulina aliingia ndani ya chumba chake huku akiwapita wapangaji wenzake bila kuwasalimia akawanyar kwa zalau kisha akaingia chumbani
"Karibu chumbani Erik"
"Mmmmmh" Erik aliguna
"Jaman shemeji si uingie tu kwani waogopa nn?"
"Okey asante hodi mpaka ndani"
" karibu shemeji"
Eriki aliingia ndani ya chumba akaakaa juu ya sofa, Paulina akaenda kuurudisha mlango kisha akaufunga kwa funguo.
Je, nini kitatokea?
USIKOSE SEHEMU YA PILI
0 comments:
Post a Comment