Kuna athari nyingi ambazo kijana anaweza kukumbana nazo kutokana na kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya ngono.
Magonjwa ya ngono yasipotibiwa mapema na kwa usahihi yanaweza kusababisha madhara yafuatayo kwa kijana.
Kwa kijana wa kike.
Kuziba kwa mirija ya uzazi ambako kunasababisha aidha mamba kutunga nje ya mfuko wa uzazi au ugumba.
Maambukizi katika mfuko wa uzazi ambako husababisha aidha kuharibika mamba mara kwa mara, kujifungua kabla ya mamba kutimiza muda wake, kuzaa motto mfu au kuzaa mtoto mwenye maambukizi ya magonjwa ya ngono. Kupata magonjwa katika viungo muhimu mwilini kama ubongo, moyo na figo.
Kansa ya kizazi Mabadiliko ya hedhi.
UKIMWI:
Kwa kijana wa kiume Maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi au kuziba mirija inayopitisha mbegu za uzazi na kuleta utasa. Kupata matatizo ya kukojoa kwa sababu ya kuziba njia ya mkojo.
Kupata magonjwa katika viungo muhimu mwilini kama ubongo, moyo na figo Magonjwa katika mishipa ya damu. Kansa ya uume Kupungua nguvu za kiume.
UKIMWI Nini kijana unapaswa kufanya Kuwa na tabia ya kutafuta taarifa sahihi za magonjwa ya ngono na kuzisoma kwa ufasaha ili kuepuka maambukizi.
Kutumia huduma za afya zilizopo ili kutibiwa magonjwa ya ngono na kuepuka madhara yatokanayo na tiba isiyo sahihi.
Kufahamu kwamba ni haki yako ya msingi kutumia huduma za afya na kupata matibabu sahihi.
Kuwa jasiri na kujiamini katika kudai haki na kuuliza maswali wahudumu wa afya kuhusu magonjwa ya ngono na matibabu yake.
Kujiunga na makundi rika na kuiomb a serikali kuweka huduma rafiki kwa vijana. Kujua kuwa ni wajibu wako kuihamasisha jamii katika kudhibiti magonjwa ya ngono.
Kuwa shujaa wa kupimwa afya yako ikiwa ni pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Kumbuka, epuka mambo yafuatayo :
Usijinunulie dawa bila ushauri wa dakatari.
Dawa utakazoshauriwa na madaktari ni za matumizi yako, usigawane na mwenzio.
Usiache kutumia dawa kama dalili zimepotea.
Maliza dozi ya dawa kama ulivyoelekezwa na daktari.
Dawa zinapatikana katika vituo vya afya bila malipo.
very good
ReplyDelete