Story:
Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18.
Wakati fundi anaendelea na kazi kumbe mmeo huyu dada alishafika. hakutaka kumjulisha mkeo, kwa nia nzuri tu ya kumfanyia suprise, kwani alikuja na mazaga zaga kibao. Hiyo aliingia kwa kunyatia hadi kwenye mlango wa chumbani kwao. Ghafla akasikia mazungumzo ya mkeo na fundi ndani. Mazungumzo yalikuwaje? fuatilia hapa chini
Mama X: Fanya haraka mme wangu amekaribia
Fundi: Nakaribia kumaliza, nisaidie kuchomeka vizuri upande wako (akikusudia chaga)
Mama X: Mbona haiingii
Fundi: Ingiza kwa upande upande
Mama X: Sukuma kwa nguvu
Fundi: Angalia usiumie
Mama X: Hamna shida imeingia
Wakati jamaa akiendelea kusikiliza mlangoni, fundi akaweza godoro juu ya kitanda na mama x akajitupa kitandani kujaribu kama kimetengamaa. mara chaga akachomoka na kuanguaka chini. Nini kilifuata
Mama x: Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiii(miguno) "my God, mbona hivi"
Fundi : Pole sana
Mama X: sasa?
Fundi: Ngoja nichomeke tena
Mama X: Yaan wewe, utaacha mme wangu afike hatujamaliza
Fundi: Usijali namaliza sasa hivi
Baada ya dakika chache, fundi akamuaga mama na kumwambia tayari, sasa naona umefurahi. Kutoka tu mlangoni akakutana uso kwa uso na jamaa amekunja ndita kama matuta ya viatu. Gues what happened?
Kitu gani kitatokea kisia toa maoni yako kama ni ww ungefanyaje?
sahare ili watu wazidi kutoa maoni yao na kumfanya admini wa page azidi kupata moyo wa kuwawekea habari nzuri zaidi
Baba na Dogo:
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo....NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.
Binti na Jamaa:
Binti: Hallo mpenzi, mambo!
Jamaa: Poa baby!
Binti: Uko wapi?
Jamaa: Mimi niko town napata lunch.
Binti: Wow! Unarudi saa ngapi? Nina njaa dear, nataka uniletee msosi.
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa, Nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne yakaangwe
pembeni, baga, piza ya samaki waweke mayonaize, coka
take away ya baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya
Wapemba na maji ya kunywa chupa kubwa ya Kilimanjaro.
Jamaa: Umesahau viti, meza, leseni, masufuria, sahani na vijiko.
Binti: Kwa nini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula, unataka kufungua hoteli??
Jamaa na binti:
MSICHANA: Mbona jana nimekupigia simu hujapokea?
JAMAA: please beby forget me.
MSichAnA: eeeh unaniambia hivo mimi?
JAMAA: nakuomba sana forget me.
MSICHANA: aya bwana poa maisha mema.
Msichana anakata simu jamaa ndo ananiuliza."sasa
sijui amekasirikia lipi?" Mi nikamwambia we zuzu
umemwambia AKUSAHAU, dah, kumbe
ningemwambiaje? hahaha, ungemwambia
ForgivE me! au Ungesema Tu NaombA nSameHe.
Msichana wa kazi:
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara..... Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatu.......
machizi wapo wengi humu duniani
ReplyDeletedaah aise
ReplyDelete😂😂😂😂
ReplyDeletekali sana
ReplyDelete😁😁😁
ReplyDeleteDuh? Nomaaaa
ReplyDelete