Katika suala la zima la kuwa na afya bora, hiyari iko mikononi mwa mtu mwenyewe. Unaweza kuamua kuishi na afya bora na unaweza pia kuamua kuishi na afya mbaya, uamuzi ni wako. Kama ilivyo kwa jambo lolote, nia, uelewa na kujituma ndiyo huwa siri ya mafanikio, hivyo hata katika suala la afya ni hivyo hivyo.
Angalizo kwa chakula unachokula:
Unene ni tatizo kubwa miongoni mwa vijana na watu wazima. Watu wengi wanakula kupita mahitaji halisi ya miili yao. Utafiti unaonesha kuwepo uhusiano mkubwa wa ulaji kupita kiasi na hatari ya kuatwa na magonjwa.
Ulaji wa chakula kiasi na chenye manufaa kiafya, kutakuhakikishia wewe na familia yako afya imara kwa miaka mingi ijayo. Ni bora kula kila siku mlo wenye faida kwa mwili wako badala ya kufanya hivyo pale unapoambiwa na daktari tu.
Ulaji wa mboga pekee (vegetarianism) unaendelea kupata umaarufu duniani kwa sababu unamuwezesha mtu kupata faida zote sawa na mtu anayekula nyama, lakini bila kuwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wowote. Pia kula matunda kwa kiasi cha kutosha, angalau kila mlo uwe na matunda na isiwe aina moja kila mlo.
Jizuie kula kupita kiasi na hakikisha unakunywa maji mengi kila siku. Wakati mwingine watu hutafsiri kiu kama njaa na kuishia kufakamia chakula wakati kilichokuwa kikihitajika mwilini kilikuwa maji tu. Hivyo tunashauriwa kutii miili yetu kwa kuhakikisha tunakunywa maji ya kutosha, hata kama hatusikii kiu, kwa sababu pale tunaposikia kiu, tayari mwili unakuwa umepungukiwa maji.
0 comments:
Post a Comment